![]() |
Advertisement |
Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli leo amehutubia wabunge wa bunge la Afrika Mashariki bungeni mjini Dodoma akizunguza katika hotuba hiyo Raisi Magufuli amesema
"Nchi zetu zina utajiri mkubwa wa rasilimali. Lakini licha ya utajiri huo bado haujawanufaisha wananchi wetu vya kutosha."
"Niwaombe wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki mlipe kipaumbele suala la maendeleo ya viwanda. Mnapotunga sheria zenu muhakikishe zinawavutia wawekezaji kuja katika nchi zetu."
Aidha raisi Magufuli amehimiza upendoo hususani kwa Wabunge na viongozi wa Afrika mashariki na kuwataka wapendane kama viongozi wa nchi zao wanavyopendana
"Umoja wetu unatakiwa uwe umoja kama tulivyo sisi Marais, Mawaziri, watendaji mpaka wananchi wote. Ifike mahali tupendane wote, sisi ni ndugu."
"Jukumu lililopo mbele yenu ni kubwa sana kwani ninyi ni wawakilishi na pia ni sauti ya wana Afrika Mashariki wote."
"Tumeweza kununua ndege sita, hatukuomba mkopo. Tunajenga meli kubwa Ziwa Victoria, hatukuomba mkopo. Tukiamua kutoka moyoni tutafanikiwa kisawasawa."
"Tafiti zinaonyesha kuwa, gharama za usafiri katika nchi zetu ni mara nne hadi sita zaidi, ukilinganisha na nchi za Asia, Marekani na Ulaya.
"Tukiamua tunaweza. Sisi Tanzania tumejaribu tukaona tunafanikiwa, ndio maana tumeweza kujenga reli ya kilomita. 700.26 kwa thamani ya trilioni 7, kwa fedha zetu wenyewe."
"Tukishirikiana vizuri 'on a win win situation' tutaweza kuijenga Afrika Mashariki yenye maendeleo."
"Ninyi Wabunge, mkiwa kama wawakilishi mnayo nafasi kubwa ya kuwaunganisha wananchi wa Afrika Mashariki. Mnalo jukumu kubwa la kuwaelimisha juu ya umuhimu wa jumuiya hii."
Aidha mbunge wa EALA nchini Uganda mheshimiwa Denisi Namala amemshukuru raisi Magufuli kwa mchango wake Imara wa kuimarisha jumuia ya Afrika Mashariki
"Tunakushukuru Rais Magufuli kwa mchango wako kuhusu kuimarisha Jumuiya yetu, Sera yako ya viwanda inapaswa kutekelezwa kwenye nchi zetu zote, hatuwezi kuendelea kama hatuna viwanda",
0 maoni: