![]() |
Advertisement |
Akizungumza baada ya kuachiwa huru Sugu amewashukuru wakazi wa Mbeya na wanachama wa Chadema kwa utulivu wao kipindi hicho alipikuwa akitumikia kifungo hicho
Joseph mbilinyi Sungu na Emmanuel Masonga walihukumiwa kifungo cha miezi mitano kwa kosa la uchochezi dhidi ya serikali ya Raisi Dkt John pombe Magufuli alipokuwa katika mkutano wa hadhara mwishoni mwa mwaka jana
Walifungwa katika Gereza la Ruanda Jijini MbeyaHukumu hiyo ilitolewa Februari 26 mwaka huu
Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe ameongoza mapokezi yao. Akiongozana na viongozi na wanasiasa wengine wa chadema
Jeshi la Magereza limeeleza kuwa, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wameachiwa huru kwa msamaha wa Rais, uliotolewa Aprili 26 mwaka huu, katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
0 maoni: