![]() |
| Advertisement |
Iringa ni mji uliopo Tanzania. Unapatikana juu ya mwamba unaoelekea Bonde la Mto Ruaha, katika eneo la nyanda za juu kusini .lakini pia Iringa ni moja ya mikoa 31 ya iliyopo Tanzania. Mkoa huu wa Iringa unaidadi ya watu wasiopungua 941,238. Na wengi wao hujishungulisha na kilimo na kusaidia kukuza Pato la Taifa
Gangilonga ni kata katika manispaa na
Mkoa wa Iringa. Kulingana na sensa ya 2002, kata ina jumla ya watu 9,680.
Unapokua mjini Iringa lazima utasikia habari kuhusu jiwe kubwa la Gangilonga linalopatikana katika kitongoji cha gangilonga mjini Iringa
Wenyeji wa kitongoji hiki waliamini kuwa jiwe hili lilikua na uwezo wa kuzungumza na hapo ndio ilikuja tafsiri halisi ya jina llililopewa jiwe hilo kwa lugha ya kihehe “ Gangi” ikiwa na maana ya jiwe na “ Longa ” ikiwa na maana Ongea ama zungumza na kufanya maana halisi ya jiwe hilo kua jiwe linalozungumza “ Gangilonga”
Inaaminika kuwa katika jiwe hili Chifu wa zamani wa kabila la kihehe Mzee Munyigumba alikua akizungumza na mizimu iliyopo ndani ya jiwe hili ikimtabilia mengi yaliyomsaidia kuimarisha utawala wake
Ata baada ya kufa mzee Munyigumba mwanae aliyerithi utawala wake Mtwa Mkwawa aliendelea kutumia jiwe hili kwa tafsiri ya mambo ya mbele kitu kilichomsaidia kushinda vita dhidi ya wajerumani na makabila mengine katika enzi za utawala wake
Mkwawa Mkuu na watumiaji wake walitumia kutathmini harakati za majeshi ya Ujerumani kutoka kituo cha kijeshi huko Iringa.
Sehemu hii ina umuhimu wa utamaduni kwasababu pia ilikuwa mahali pa kuabudu mababu na kuomba mwongozo.
Marejeo ya 'mawe ya kuzungumza' yanatoka kwenye hadithi za mababu na sauti hizo kutoka kwenye mwamba.
Pia, inasemekana kuwa Mkwawa na baraza lake la vita limewatafisha nyasi maalum na mwelekeo wa moshi ulionyeshwa wapi adui zao walikuwa wanatoka.
Manispaa sasa imeboresha kivutio hichi cha utalii kuna walinzi wa usalama kusaidia wageni. Kuna malipo ya kuingia kuanzia 5000 TSH (wasio wakazi) hadi 2000 TSH (wakazi). Muggings / wizi si suala tena na wageni wanaweza kupanda juu ya mwamba (ugumu wa kati) na kuchunguza 'Nchi ya Mkwawa' salama.
unapokua juu kabisa ya jiwe hili unapata fursa kuona vizuri mandhari ya kitu kinachowavutia watalii mbalimbali ndani na nje ya nchi kutembelea kitongoji hicho cha Gangilonga


0 maoni: