![]() |
Advertisement |
Wachezaji wa Manchester United ambao walishindwa kufanya vizuri katika mchezo wa Ligi Kuu ya dhidi West Brom hawatacheza mchezo wa FA dhidi ya Tottenham, amesema kocha wa timu hiyo Jose Mourinho.
Mashetani wekundu walishindwa kufanya vizuri katika mchezo huo ambapo Manchester united ilifungwa 1-0 na West Brom huko Old Trafford siku ya Jumapili, na kupelekea Manchester City kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza
United atashuka tena dimbani siku ya jumatano kukipiga dhidi ya Bournemouth kabla ya kukabiliana na Spurs.
Meneja huyo kutoka nchini Ureno alisema "baadhi ya wachezaji ambao walicheza dhidi ya West Brom "hawana nafasi" katika mchezo dhidi ya Tottenham utakaopigwa katika uwanja wa Wembley.
Aliongeza kuwa mchezo dhidi ya Bournemouth kwenye Uwanja wa Vitality itakuwa "nafasi kwa wachezaji wengine watakao cheza vizuri kupata nafasi katika mchezo dhidi ya spurs
Alipoulizwa kufafanua kama alimaanisha wale waliofanya vibaya dhidi ya Baggies sasa hawatawakabili Spurs, Mourinho alisema: "Ndio.
"Ni vigezo gani kwa meneja anatumia kuchagua timu?
"Ninajua tu kiwango cha mmoja mmoja : ndiyo njia ninayotumia"
Mchezaji Ander Herrera aliondolewa katika mchezo dhidi ya West Brom, wakati Paulo Pogba alibadilishwa katika dakika ya 58.
Kuhusu Pogba, Mourinho alisema: "Hakuwa yeye tu na alikuwa na kadi ya njano, kwa hiyo alikuwa katika hali ngumu zaidi kuliko wengine.
"Na kucheza na wachezaji wawili tu wa midfield, huwezi kucheza na mchezaji mmoja katika hatari ya kutoweza kufanya makosa
"Unaweza kufanya hivyo ikiwa timu yako haijafungwa , lakini timu yetu ilikuwa imeshapoteza na mchezo wetu ulikuwa mgumu, kwa hiyo tulipoteza mipira mingi.
"Paulo pogba alitolewa nje kwa sababu ya kadi ya njano, aliyopewa katika mchezo huo Siku ya jumapili
0 maoni: