Jumatano, 11 Aprili 2018

Magufuli:kama ulivyonibeba sitokuangusha

ad300
Advertisement

IKULU, DAR: Leo April 11, 2018 Rais Magufuli ameizindua taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo chini ya Rais Mstaafu Jayaka Kikwete

Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali inahusika na mambo manne; Utawala Bora, Maendeleo ya Vijana, Afya ya Mama na Mtoto na Maendeleo ya Wakulima Wadogo Wadogo
-
Akiongea katika uzinduzi huo Rais Mstaafu Kikwete amesema kwa sasa Taasisi hiyo itaanza kijishughulisha na masuala ya Afya kwanza pia Raising Kikwete amemshukuru Magufuli kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo na kusema kuwa

"Mheshimiwa Rais, uliopokubali ombi langu la kuwa mgeni wa Rasmi kwenye Uzinduzi wa Taasisi yetu.. umetupa heshima kubwa ambayo daima tutaikumbuka. Kwa lugha ya mjini wanasema ‘umetupa kiki’ Umeipa kiki (Taasisi) ambayo si ya kawaida"

Naye Rais Magufuli amesemsifu na kumshukuru Kikwete kwa kuanzisha Taasisi hiyo na kuahidi kwamba Serikali ya awamu ya 5 itafanya kazi bega kwa bega na Taasisi hiyo

Rais Magufuli kwa Jakaya Mrisho Kikwete. Nitaendelea kukushukuru kila tutakapokutana. Ukichukia nitakushukuru, ukifurahi nitakushukuru.. Kwa sababu ni wewe uliyesimama imara na mpaka leo mimi ni Rais

Napenda uamini; kama ulivyonibeba, sitokuangusha!


"Nakupongeza  hata baada ya kustaafu umeamua kuendelea kulitumikia taifa letu
Naona umezidi kupendeza, na mimi sitaongeza hata dakika moja kwa sababu nimeiona faida ya kustaafu"

Aidha, Magufuli ameomba watu mbalimbali ikiwemo Mabalozi wamuunge mkono Kikwete katika Taasisi hiyo kwa kuwa anamuamini.

" Ninawaomba wadau na hata Mabalozi mbalimbali muiunge mkono Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete. Ninamuamini!"

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: