Ijumaa, 13 Aprili 2018

Mrithi wa Tundu lissu TLS

ad300
Advertisement

Arusha. Mchuano mkali wa mrithi wa Tundu Lissu katika nafasi ya urais wa chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) unaendelea jijini hapa.

Katika hatua ya sasa, mnyukano unaonekana kuwa kati ya mawakili Fatma Karume na Godwin Simba Gwilimi.

Fatma Karume anaonekana kujipanga akiwa na timu ya wanasheria wasiopungua 10 waliovaa fulana zinazompigia kampeni huku timu ya Gwilimi ikiendelea na kampeni kali.

"Naomba ubadili msimamo wako leo najua upo upande ambao upo na hautajutia uamuzi wako,"amesema mmoja wa wagombea.
Hata hivyo Wakili Addo Novemba amesema anasikitishwa na hali ya sasa ya TLS ambayo anaifananisha na chama cha siasa.

Amesema mtizamo wa sasa hauoneshi kama ni chombo cha kitaaluma bali kimeelemewa na itikadi za kisiasa ambazo zinakinyima uhuru wake.
Katika hatua nyingine Rais mstaafu wa TLS, Fransis Stolla ambaye amekua kiongozi wa mkutano wa asubuhi aliwatangazia wajumbe kuendelea kuchangia fedha za matibabu za Rais wa TLS, Tundu Lissu ambaye yupo kwenye matibabu nchini Ubelgiji.

Kwa upande mwingine. Jaji Kiongozi, Ferdinand Wambali amesema wanafanya kila linalowezekana kukomesha rushwa kwenye mfumo wa sheria.
Amesema hayo leo Aprili 13, 2018 alipofungua mkutano wa mwaka wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), jijini Arusha.

Jaji Wambali amesema rushwa inawanyima haki wananchi.
Amewataka wanasheria kujitathmini kama malengo ya kuanzishwa taasisi hiyo yanaakisi shughuli zao sasa kulinganisha na idadi kubwa iliyopo ya wanasheria.

Jaji Wambali amesema katika kuharakisha huduma za kisheria mfumo wa Mahakama umeboresha utendaji kazi kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) ili kusaidia kuharakisha haki kupatikana.

Katika ufunguzi huo, Jaji Wambali amezindua kitabu toleo la pili la hali ya kisheria nchini kilichoandaliwa na TLS.
Makamu wa Rais wa TLS, Godwin Ngwilimi amesema wakiwa chombo cha kitaaluma wana wajibu wa kujisimamia badala ya kupangiwa kanuni za kufuata ikizingatiwa yapo mapendekezo yanayotakiwa kutolewa uamuzi katika ngazi ya Serikali ambayo yamewasilishwa muda mrefu lakini Serikali imekaa kimya.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: