![]() |
| Advertisement |
Arsene Wenger amesema licha ya kupata presha kubwa kutoka kwa mashabiki, kamwe hataachia ngazi.
Mashabiki wa Arsenal wamemshikia mabango wakimtaka Wenger ajiuzulu baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-0 na Manchester City Jumapili iliyopita.
“Nimesikia kelele zote zinazopigwa dhidi yangu kuhusu mkataba wangu, nimepuuza,” alisema kocha huyo Mfaransa.
Mkataba wa Wenger unamalizika mwakani, lakini mashabiki wa klabu hiyo wanataka aondoke mwishoni mwa msimu huu.
Licha ya kutoa kauli hiyo, vigogo wa Arsenal walitarajiwa kuanza kupitia rekodi yake na taarifa za awali zilidai wakati wowote anaweza kutupiwa virago.
Wajumbe wa Bodi Arsenal walimuweka kitimoto Wenger muda mfupi baada ya kumalizika mchezo dhidi ya Man City.


0 maoni: