Jumatatu, 12 Machi 2018

Uvccm wakagua utekelezaji wa ilani Temeke

ad300
Advertisement

Mwenyekiti Umoja wa Vijana Wa CCM (UVCCM)  Mkoa wa Dar es salaam Bw. Mussa Kilakala leo ameanza ziara kutembelea Wilaya za  Mkoa wa Dar es salaam ambapo leo ameanzia Wilaya ya Temeke  na  amekutana na kuzungumza  na  vijana na watumishi wa Manispaa  hiyo.



Kilakala amesema kuwa  lengo la Ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi na pia kuangalia Umoja wa Vijana unavyofanyika fanya kazi zake.

Akizungumzia upande wa ujasiriamali ameipongeza Wilaya hiyo kwa kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wananchi wasiopungua elfu moja na ameendelea kusema kuwa wajasiriamali hao ni lazima wapewe mitaji ili wautumie ujasiriamali wao katika kuzalisha.



''Sehemu ya pekee ambayo wanaweza kuanzia kama Vijana ili kupata mitaji hiyo ni kutoka kwenye Halmashauri ambapo Vijana wanatakiwa wapewe asilimia 5% ya Mapato ya ndani na ni jukumu lao kama Umoja kutembelea Halmashauri na Idara mbalimbali ili wajue utekelezaji wa Ilani juu ya asilimia 5% hiyo na namna ambavyo Vijana wanaweza kunufaika nayo, amesema Kilakala

Hata hivyo  Kilakala amesema Mkoa wa Dar es salaam umezindua mfumo maalum wa kutambua Vijana wote,ujuzi wao pamoja na shughuli wanazofanya ili takwimu sahihi ziweze kuandaliwa na Vijana wote wanufaike sawasawa.



Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaniva amewataka wa pokea vijana na hao na kuwa hakikisheni kuwa ilani ya CCM katika Wilaya Temeke inatekelezwa ipasavyo na kwa upande wa usalama wameimeimarisha ulinzi na matukio ya uharifu yamepungua, na kwamba Halmashauri hiyo inatekeleza miradi ya maendeleo.

Ziara hiyo ambayo ambayo imehitimishwa, iliambata na viongozi mbalimbali wa UVCCM Mkoa na Wilaya ambapo walilidhishwa na namna ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyotekelezwa katika wilaya ya Temeke kwakuwajali vijana kwani wamehakikisha 5% wananufaikanazo vijana ambazo zimetengwa kwa ajili ya kuwaendeleza kwa kipato.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

Maoni 1 :