![]() |
| Advertisement |
Mtandao wa wanafunzi Tanzania TSNP umeeleza kufungua shauri mahakama kuu ili kulitaka jeshi la polisi limuachie au kumfungulia mashtaka mwenyekiti wa mtandao huo Abdul Nondo hatua hiyo imefuatia kushikiriwa na jeshi la polisi kwa mwenyekiti huyo ambae inasadikika kuwa alijiteka Na siku ya pili yake kupatikana katika mji wa Mafinga Jeshi la polisi hivi karibuni lilieleza kuwa litamfikisha mahakamani Abdul Nondo pindi shauri lake litakapo kamilishwa na Jeshi la hilo Mtandao wa wanafunzi Tanzania umeeleza kupitia Mtandao wake wa tweeter na kusema kuwa
"Shauri tulilolifungua mahakama kuu la kulitaka jeshi la polisi aidha limuachilie huru au limshitaki Abdul Nondo mwenyekiti wa TSNP limepangiwa Jaji SAMEJI na litasikilizwa 21/03/2018. Nondo anashikiliwa na polisi "mahali kusikojulikana" kwa zaidi ya siku 10 sasa #FreeAbdulNondo."
Aidha mtandao wa wanafunzi Tanzania umewashukuru watanzania wrote waliopaza sauti kumtetea mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo na pia limeelezakuendelea kuuamini muhimili wa mahakama katika utendaji wake wa kazi na kuamini haki kupatikana
"Tunawashukuru watanzania wote wanaoendelea kupaza sauti za kupinga ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu unaofanywa dhidi ya Abdul Nondo bila kujali kama anahatia au hanahatia
Shukrani kwa @Advocate_Jebra na mawakili wote wanaoshughulikia "TATIZO" hili. #FreeAbdulNondo
"Tunaamini, mahakama itatenda haki kwa mujibu wa sheria. Kesi itasikilizwa 21/3/2018 saa3:00 asubuhi Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam mbele ya Mhe. Jaji Rehema Sameji."


0 maoni: