![]() |
| Advertisement |
Mkali wa hiphop na Rapa Stamina amefunguka na kushangazwa juu ya kufungiwa kwa wimbo wa kibamia walioufanya msanii Roma mkatoliki kama kundi la Rostam
Stamina amefunguka hayo baada ya kusikia Roma Mkatoliki amefungiwa kujihusisha na sanaa sababu ikiwa ni kutofanya marekebisho ya wimbo wao wa Kibamia na kusema kuwa awali walipoongea na Waziri huyo aliwapa miezi sita ya kufanya marekebisho ya wimbo huo sasa iweje amechukua maamuzi ili hali hata muda ambao walipewa haujakwisha.
Akiandika kupitia ukurasa wake wa Instagram stamina amewapa lawama balaza la Sana'a la taifa BASATA na kuhoji kama inakuza au inabomoa Sana'a stamina amesema
"Kiba_100 Ilitoka Tarehe 22November
Na Basata Roma Tuliitwa Tarehe 6December
Na Mh.Waziri Akasema Wametupa Miezi Sita!! Na Leo Ndio Kwanza Tarehe 1 Mwezi Wa Tatu!! MBONA MIEZI SITA BADO!!??? AU MIEZI SITA YA TANZANIA IKO TOFAUTI NA KALENDA YA DUNIA NZIMA?? MNA TATIZO GANI NA WASANII WETU BASATA NA WIZARA!? Mnakuza Au Mnaua Sanaa!??"
Stamina na Roma ni wasanii waliounda kundi la Rostam ambalo mbaka sasa limefanikiwa kuteka soko la muziki wa hiphop kutokana na ushirika mzuri uliopo kwa ya wasanii wote wawili.Roma na stamina mbaka sasa wameshatoa nyimbo mbili. Ambapo mmoja umefungiwa na BASATA kutokana na kukosekana kwa maadili katika wimbo huo


0 maoni: