Ijumaa, 2 Machi 2018

Sosopi afunguka kufungiwa kwa Roma

ad300
Advertisement

Mwenyekiti wa balaza la vijana chadema BAVICHA Patrick ole sosopi amesema kuwa kumfungia msanii miezi sita ni sawa na kumuua  hatua hiyo imekuja kufuatia kufungiwa kwa nyimbo kadhaa na kusimamishwa kufanya mziki kwa Muda  wa miezi sita msanii Roma mkatoliki "Sosopi amesema hayo Leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

"Kumfungia msanii bila kazi ni mauwaji
Kwasababu msanii huyu anasomesha
Msanii huyu anategemewa na ndugu
Msanii huyu anafanya shughuli zake na ndipo palipo mwajiri
Kitendo cha kumwambia asifanye kazi maana yake asile maana yake asisomeshe maana yake a stop maisha yake ya kawaida yakibinadamu kitu ambacho kitampelekea aidha awe kibaka au awe mwizi"

Kwa upande mwingine sosopi amemtupia mzigo wa lawama naibu waziri  wa habari vijana utamaduni na michezo Magdalena shonza na kusema kuwa waziri huyo anamamlaka ya kuwasimamia BASATA na si kutoa uamuzi

Lakini pia Patriki ole sosopi amesema kuwa BASATA wamefanya uzembe kuchelewa kuzifungia nyimbo hizo kwani zilikwisha toka na kwasasa hazina mvuto tena kwa jamii

Ikumbukwe kuwa Siku chache zilizopita Naibu waziri  wa habari vijana utamaduni na michezo alitangaza kuzifungia nyimbo kadhaa za wasanii wa bongoflava kutokana na kukosekana kwa maadili katika nyimbo hizo.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: