Jumamosi, 17 Machi 2018

Okwi tunauwezo Mkubwa wa kuichapa Al masry

ad300
Advertisement



Emmanuel Okwi, amesema kuwa kitaalamu muda wa kuzoea hali ya hewa huwa saa 48 tu sawa na siku mbili, hivyo wana asilimia kubwa za kuifunga Al Masry hapa kwao Port Said katika mchezo wao wa leo.

Simba leo Jumamosi usiku inarudiana na Al Masry katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Port Said jijini hapa.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Okwi alisema kwa saa 48 walizokaa hapa wameshazoea hali ya hewa na wanatambua Al Masry ni timu kubwa ila hawaiogopi kwani hata Simba ni timu kubwa na wako hapa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

“Nashukuru hali ya afya za wachezaji wenzangu ziko safi na kila mmoja ana hamu ya kushinda hivyo tutapambana kwa kila hali ili tuweze kushinda, saa 48 tulizokuwa hapa zimetufanya tuzoee hali ya hewa.

“Siyo jambo rahisi kushinda ugenini ila inawezekana sana kwetu kufuatia wenzangu wote kuonekana kuwa na morali ya kutosha kwani sisi ni wanajeshi tumekuja kupambania ushindi,” alisema Okwi.

Kwa upande wa John Bocco, yeye alisema yuko fiti na wenzake wamemhakikishia ushindi hivyo watafanya iwezekanavyo ili waweze kuwaletea Watanzania ushindi.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: