![]() |
| Advertisement |
Baada ya nyimbo kadhaa za wasanii wa muziki wa kizazi kipya kufungiwa Msanii na mkali wa rap kutoka kundi la weusi Nikki wa pili ameeleza na kusema kuwa nyimbo za matusi ziliimbwa kwenye kampeni za uchaguzi akiandika kupitia ukurasa wa tweeter Nikki amesema
"Tukizungumzia nyimbo za matusi bana zilitoka wakati wa kampeni, bwana we matusi ya nguoni, tena yakitukana watu wazima na heshima zao, hapa walezi walikaa kimya.
Lakini pia Nikki wa pili amewataka BASATA kutojikita kufungia nyimbo za wasanii tu kwa sababu za kimaadili Bali isimamie zaidi maslahi yao
Basata kama walezi, msisahau pia kuyalinda maadili yetu ya kiuchumii, kama mlezi alafu watoto wako wanakua wanaishia kufa, inamanisha hawa kulelewa vizuri kiuchumi
Hii karibuni nyimbo kadhaa za wasanii wa kizazi kipya zilifungiwa kutokana na kukosekana kwa maadili katika nyimbo hizo huku Msanii ROMA Mkatoliki akifungiwa kufanya muziki kwa muda wa miezi sita


0 maoni: