Jumatatu, 5 Machi 2018

Nape akemea ulevi wa Madaraka

ad300
Advertisement

Mbunge wa jimbo la Mtama kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Nape Nnauye amelaani mfumo wa baadhi ya viongozi wanaobadili mfumo wa ukomo wao wa utawala na kujiongezea miaka au mihula ya kutawala.

Nape amefananisha kitendo hicho sawa na ushetani na kuwataka vijana wa Kiafrika kupambana  kupinga mfumo huo ambao unakandamiza demokrasia. Nape nauye kupitia ukurasa wake was tweeter amesema kuwa

“Huu ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani na lazima upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla utaratibu huu haujaota mizizi na kusambaa! Hii ni zaidi ya kansa“

Baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda na Rwanda tayari nchi hizo zimebadili mfumo wa ukomo wa urais madarakani ambapo Rais atahudumu kwa miaka 7 na Uganda wamefuta kabisa hadi ukomo wa umri wa Rais kustaafu.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: