![]() |
| Advertisement |
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetolea ufafanuzi kuhusu kile kinachoitwa kutekwa kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Nchini TSNP, Abdul Nondo.
Akizungumza na Wandishi wa Habari Kamanda wa Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa amesema mnamo Machi 7, mwaka huu waliletewa taarifa kutoka kwa wenzao wa Iringa ambapo walithibitisha kupatikana kwa mwanafunzi huyo akiwa mzima huku akiwa hajaripoti kituo chochote cha Polisi.
Mambosasa amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalumu kwa kushirikiana na wenzao wa Iringa walithibitisha kuwa Nondo hakutekwa bali alijiteka ambapo mawasiliano ya jumbe za simu yake zinaonesha kuwa alikuwa akiwasiliana na mpenzi wake aliyepo mkoani humo.
Kijana huyu ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hakutekwa wala kushikiliwa bali alijiteka mwenyewe kwa nia ama ya kutafuta umarufu au kwa sababu ambazo anazijua mwenyewe,
"Tulikuwa na mashaka huenda alikuwa na matatizo ya akili yaliyopelekea akayafanya haya. Lakini alipopimwa, taarifa ya daktari ilionyesha kwamba hana hitilafu yoyote ya kiakili. Ni mzima wa afya na haya ameyafanya kwa makusudi kwa sababu anazozijua mwenyewe." Alisema Kamanda Mambosaaa
Lakini pia jeshi la polisi linaendelea kumshikiria kijana huyo na linakamilisha taratibu za kisheria ili kumfikisha mahakamani na kutoa onto Kali kwa watu kwenye lengo kama hili
"Huyu tunaendelea kumshikilia, wakati tunakamilisha taratibu za kisheria, tumpeleke mahakamani ili akajibu shtaka hilo la uzushi na uongo uliopelekea taharuki kubwa."
" Jeshi la Polisi tunaendelea kutoa onyo kwa sababu hatutomuhurumia mtu yeyote ambaye anatafuta umaarufu kwa kuzua taharuki na wala hatutowapa nafasi ya kuharibu amani ya Nchi," amesema Kamanda mambosasa



0 maoni: