Jumamosi, 17 Machi 2018

Makonda Amsifu Meya wa chadema

ad300
Advertisement

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtuma meya wa jiji kuzungumza na viongozi wake wa chama(Chadema) kufikiria upya kuhusu hali ya usalama katika jiji hilo ili kufanikisha ukuzaji wa sekta ya utalii katika jiji hilo.

“Mstahiki meya wa jiji, leo tunazindua utalii wa ndani na tumemuita waziri wa Tamisemi atuzindulie, kawaulize ndugu zako wale akina Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema) na akina nani wale, waulize...wakifanya vurugu, hawana watalii watapita mji gani?”Amehoji Makonda leo Machi 17, 2018 wakati wa mkutano wa kuzindua utalii wa ndani katika mkoa huo.

Katika hatua nyingine, Makonda ametoa maagizo manne katika kufanikisha utalii wa ndani katika jiji hilo akisema, kwanza ni lazima kuhamasisha utalii huo, kuendeleza usafi katika jiji hilo, kuboresha vituo vya mabasi yaendayo mikoani.

Katika hatua nyingine, Makonda ameahidi kuzindua viwanda 200 katika jiji hilo hapo baadaye badala ya viwanda 100 vilivyoagizwa na Serikali katika kila mkoa

“Ulitupatia maelekezo ya kila mkoa viwanda 100, mie nakuahidi , nitakualika mwenyewe kuzindua ujenzi wa viwanda 200 kwa wakati mmoja, tumeshapata wawekezaji na sasa tuko kwenye mchakato wa kukamilisha suala la ardhi,”amesema Makonda.

Awali, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana ametaja mipango kadhaa iliyoanza kutekelezwa na jiji hilo katika kukuza na kuimarisha sekta ya utalii.

 Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemmwagia sifa Meya wa Jiji hilo, Isaya Mwita akisema ni kiongozi atakayeendelea kung’aa katika uongozi wake kutokana na kazi anazofanya kwa ajili ya Watanzania.

Makonda ametoa kauli hiyo leo Machi 17, 2018 wakati wa mkutano wa kuzindua utalii wa ndani katika mkoa huo, akisema meya wa aina hiyo ni lazima kupata ushirikiano wa ofisi yake tofauti na mameya wanaobakia kumtukana rais.

Katika mkutano huo, RC Makonda amesema Mwita ni mwanasiasa mwenye dhamira njema ya kuwatumikia Watanzania, kama ilivyo kwa dhamira ya rais John Magufuli.


“Pia niendelee kukupongeza Meya wa jiji la Dar es Salaam, kaka yangu na ndugu yangu, na timu yako ya madiwani kwa kazi kubwa unayoifanya, katika jiji tunao madiwani wa vyama vyote ila meya wetu wa jiji ni wa tofauti, ni meya anayetazama maendeleo, anayetaka kazi, tangu nifahamiane naye kila anapokuja ofisini kwangu, ni mpango wa namna gani tunafanya kazi, ndiyo maana ataendelea ‘ku-shine’ kuliko mameya wengine wa upinzani,”amesema.

Amesema kundi la mameya wanaoendelea kumtukana rais, litaishia kuhesabu matusi tu na mwisho wake sheria itachukua

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: