![]() |
| Advertisement |
Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe ameshindwa kuvumilia matukio mbalimbali yanayojitokeza katika ardhi ya Tanzania na mwisho ameamua kuandika barua yenye hoja binafsi kwa Katibu wa Bunge ili kuundwe kamati ya teule ya uchunguzi kupitia Mtandao ya kijamii wa tweeter Bashe aliandika
Leo asubuhi nimewasilisha Kwa Katibu wa Bunge barua ya kusudio la kuwasilisha Hoja Binafsi ya kuunda Kamati Teule ya Bunge kuchunguza matukio mbalimbali yanayoonesha kutishia umoja, usalama na mshikamano wa Taifa letu.
Lakini uamuzi Hui ulipingwa vikali na Mbunge wa Arusha mjini Godbless lema huku akimshutumu Bashe nakusema kuwa ni mnafki na mwoga
Unafiki.Tunahitaji Kamati teule kujua mikutano ya siasa imezuiwa?au watu wanatekwa na kuuwawa na kwamba uhuru wa demokrasia na Bunge umekufa?acha uoga kemea Serikali ya Chama chako,halafu hiyo Kamati teule ipeleke taarifa Bunge gani?Nzega kuna nini maana Kigwangala naye kama wewe
Lakini pia bashe hakuishia hapo kupitia alimjibu Godbless Lema na kumwambia kuwa
Hili ndo Tatizo la Viongozi wa aina yako Unafhani kukemea watsup or tweeter ndo utatatua tatizo Bunge limekufa kukemea ndo litafufuka Kabla hujakemea Tangaza hadharani Umeshindwa kutumiza wajibu Wako ama Jiuzulu ,Unafiki ni huu Wako kushindwa kutumia Muhimili wa Kisheria
Kwa upande mwingine, hoja ya Bashe imeungwa mkono na Mbunge wa kigoma mjini kupitia chama cha ACT wazalendo na kusema kuwa uamuzi wa Bashe ni sahihi na atauunga Mkono
Uamuzi huu wa Mbunge wa Nzega Mjini ni uamuzi sahihi unaopaswa kuungwa mkono na kila mmoja wetu. Kwame Nkrumah alipata kusema “ One Struggle, Many Fronts “. Kila mtu anayefanya lolote kusaidia kuiokoa nchi yetu aungwe mkono bila kujali Chama chake. Nitaunga mkono hoja hii ikija
Lakini zitto aliongeza na kusema kuwa
Kwa maana hiyo sote tutoke Bungeni? Maana ndio Bunge hilo hilo tumo. Wakati mwengine huwasilishi hoja ili ipite ( hoja zetu wapinzani nadra kupita), unawasilisha kuweka rekodi ya kupinga haya mambo. Mtume Muhammad anasema ‘ kama huwezi kuzuia na kukemea uovu, nuna basi ‘
Hivi karibuni kumekuwa na matukio kadhaa ya watu kupotea,kutekwa na kuuwawa bila wahusika kukamatwa na vyombo vya sheria.


0 maoni: