Ijumaa, 2 Machi 2018

ACT yamkataa kalumuna yasema ili shamtema siku nyingi

ad300
Advertisement

Mkuu wa itikadi na uenezi wa chama cha ACT wazalendo Addo shaibu amesema kuwa yeyote anayetaka kuhama ACT wazalendo ahame na aende kwa amani.

"Yeyote anaetaka kutoka katika chama chetu sisi tunamwambia kila la kheri, sasa huyo anaejiita katibu wa chama Mkoa wa Dar es salaam tayari alishajiunga na ccm sasa na leo tena anatangaza kujiunga na chama hicho CCM inawatu wanajiunga mara tatu, tatu au vp?"

Hata hivyo Baadhi ya watu waliotangazwa kwenye orodha ya wanachama wa ACT Wazalendo waliokihama Chama hicho na kuhamia CCM wamekana kuhama chama hicho, orodha hiyo imesomwa leo mbele ya waandishi wa habari na Kalumuna Ernest aliyejitambulisha kuwa Katibu wa chama hicho.

Hii ni Mara ya pili kwa ndugu Kalumuna kutangaza kukihama Chama cha ACT Wazalendo ambapo mara ya kwanza alitangaza kufanya hivyo kwenye kampeni za CCM katika Jimbo la Kinondoni.

Vile vile Chama cha ACT Wazalendo kupitia kwa Afisa Habari wake Abdallah Khamis alieleza kuwa Chama hicho kilishamuondoa kwenye ukatibu wa Mkoa na Kamati Kuu miezi mingi nyuma.

Mmoja wa watu waliotajwa Kwenye orodha ya leo iliyosomwa na Kalumuna, Robert Kihiri ambaye alitajwa Kama Mwenyekiti wa Vijana wa Jimbo la Ubungo amesema “Wapuuzeni hao watu, ni wahuni. Wamenifuatilia mimi kwa simu hadi kwangu wamefika kunishawishi nijiunge CCM, nimekataa. Mimi bado ni mwanachama wa ACT Wazalendo na sina Shaka na mwenendo wa Chama chetu. Sijakihama Kama wanavyodai,” amesema Robert Kihiri.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: