Alhamisi, 12 Aprili 2018

Zitto aitaka serikali kueleza kupotea kwa Diwani wa Kakonko

ad300
Advertisement


Dodoma. Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT -Wazalendo), Zitto Kabwe amemtaka waziri wa Tamisemi kulitafutia ufumbuzi suala la kutoweka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kakonko, Simon Kangue.

Amesema hayo bungeni leo Aprili 12, 2018 alipochangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, yenye wizara za Tamisemi; na Utumishi na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Habari zinazosambaa Kibondo tayari ameuawa. Tunataka maelezo ya mtu huyo, sisi watu wa Kigoma ni Kigoma kwanza kabla ya kuwa Watanzania naomba hilo mlielewe,” amesema.

Zitto amesema mara ya mwisho kuonekana mwenyekiti huyo aliitwa kwa mkurugenzi na kukutana na ofisa usalama wa wilaya.

Amesema tangu siku hiyo hajulikani alipo mwenyekiti huyo licha ya jitihada za kumtafuta kufanyika.

“Familia imechukua hatua mbalimbali, imelalamika na sisi wajumbe wenzake tumehoji kwenye vikao, hakuna maelezo yoyote kutoka serikalini,” alisema Zitto.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: