Jumapili, 8 Aprili 2018

TUCTA yakazia ombi la Msukuma

ad300
Advertisement

Akiongea Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya amesema watumishi wenye elimu ya darasa la Saba wameajiriwa kwa muda mrefu na wengi wao umri wa kufanya kazi umeelekea ukingoni na kwa mantiki hiyo wameitaka Serikali kuwarudisha Kazini bila kupoteza haki zao za kiutumishi kwa kipindi chote walichofanya kazi.

Pia wameitaka Serikali kuangalia upya ongezeko la mishahara na kupandishwa madaraja, vyeo kwa watumishi wa umma.

Naye katibu wa Baraza, Yahya Msigwa amesema baadhi ya watumishi Tanzania wameanza kukata tamaa kwa kukosa motisha akitolea mfano wa ng'ombe asielishwa vizuri asivyoweza kutoa maziwa ya kutosha.

TUCTA pia wameeleza kusikitishwa na kucheleweshwa kwa malipo ya wastaafu kwa baadhi ya mifuko ya jamii pamoja na malimbikizo ya mishahara kwa Wafanyakazi na watumishi katika taasisi mbalimbali.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: