Jumamosi, 7 Aprili 2018

Raisi Magufuli:Nyumba za polisi ndizo zimenipa mke

ad300
Advertisement

Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo ametoboa siri kuwa mke wake, Janeth alikuwa ni mtoto wa polisi.

Ameyasema hayo leo Aprili 7 wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za polisi mjini Arusha na kusema baba mkwe wake alikuwa sajenti wa polisi.

“Nyumba za polisi ndizo zimenipa mke kwa hiyo nyumba za polisi ninazifahamu, huyu mke wangu niliye naye alikuwa mtoto wa polisi, marehemu baba yake hakuwa na cheo kikubwa alifariki akiwa sajenti,” amesema.

Ameongeza kuwa, “Ingekuwa nazindua Moshi, angenionyesha nyumba walizokaa lakini za Oysterbay alizoishi alishanionyesha na za Ukonga na za sehemu nyingine. Kwa hiyo maisha ya polisi ninayafahamu.”

Aidha raisi Magufuli Amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kuhakikisha polisi hao wanaingia kwenye nyumba zao kesho.

"Hawa waliounguliwa hizi nyumba, kesho waingie kwenye nyumba zao ambazo zimemalizwa kujengwa kwa sababu huwa najua saa zingine Polisi wanawezwa kuletwa wengine maofisa, waliokuwemo wakaambiwa hapana.

Nataka waliounguliwa nyumba, ndio waingizwe humu"

Lakini pia Rais Magufuli amezindua kituo cha polisi cha  Kidiplomasia na Utalii jijini Arusha. Kituo hicho kitakuwa kinawahudumia watalii, mabalozi na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu za serikali wa ndani na nje ya nchi.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: