![]() |
| Advertisement |
Askofu Isaac Amani Massawe ambaye leo amesimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Arusha. Alizaliwa Mango, Moshi, Juni 10, 1951 na kupata upadri Juni 29, 1975. Aliteuliwa kuwa Askofu mwaka 2007 na kisha Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Disemba 27, 2017.
Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu Jijini Arusha na kuhudhuriwa na Raisi was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Mkewe, Mama Janeth Magufuli wamempongeza Mhashamu Isaac Amani baada ya kusimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha.
Hatua hii ni Muhimu kwa raisi Magufuli katika kurejesha mahusiano na maaskofu yaliyopatwa doa hivi karibuni kufuatia kutolewa kwa nyaraka mbalimbali zenye maudhui ya kuikosoa serikali
Licha ya kukosolewa, rais Magufuli alipuuzilia mbali mbali nyaraka za maaskofu zilizotolewa wakati wa kuanza kwa msimu wa Pasaka akisema hazina msingi wowote ule.Aliendelea kwa kusema pia kwamba mbona hakuna aliyetoa waraka wakati mauwaji ya Kibiti yakiendelea.
Rais Magufuli amesema hayo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa rada za kiraia uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Majibu yake kwa nyaraka za maaskofu aliyatoa wakati akiwapongeza wasaidizi wake, mawaziri, viongozi wa ulinzi na usalama pamoja na wasaidizi wengine, ambao amewasifu kwa kuendelea kutimiza majukumu yao...
"Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ndio maana tuko salama leo, ilifikia mahali hata kwenda Kibiti tu ni kazi. Hatukuona mtu yeyote analaani," alisema Dkt Magufuli.


0 maoni: