![]() |
Advertisement |
Kauli saba muhimu za Mbunge Peter Msigwa wa CHADEMA kwa Rais Magufuli kuhusu hali ya nchi.
Rais Magufuli aliamini kuwa, sifa kuu ya kuwa Kiongozi ni kuwa Kiongozi wa wanyonge pekee. Mbaya zaidi aliamini kuwa, umaskini na shida za wanyonge zitakwisha kwa kuwabana na kuwachukia matajiri.
Rais Magufuli anakumbuka shuka wakati tayari kumeshakucha. Miaka miwili iliyopita, kwa ushahidi wa kauli zake mwenyewe, alikuwa anawaona matajiri ambao wengi wao ni wafanyabiashara mithiri ya mashetani.
Wakati ule niliandika kwamba, ujinga hauondoki kwa kumchukia mwenye akili na umaskini hauondoki kwa kumchukia tajiri. Kuhesabu dhambi za mwenzako hakukufanyi wewe kuwa Mtakatifu.
Ni kwa bahati mbaya, Rais Magufuli hakujua kwamba hawa matajiri, wafanyabiashara na sekta binafsi kwa ujumla wana mchango mkubwa katika kufikisha bidhaa, huduma na kuchochea maendeleo ya watu wa kipato cha chini.
Bado alikuwa kwenye mtazamo na imani ileile ya miaka ya 1961 ya kuamini kwamba, Serikali inaweza kufanya kila kitu yenyewe chini ya uongozi wake hodari.
Mambo mengi yanayolalamikiwa na wafanyabiashara, yanawezekana kabisa kushughulikiwa na Mamlaka, Idara au hata Wizara husika, lakini Rais Magufuli kama kawaida yake kajitwika yeye.
Tuendelee kumshauri ajiuzulu ili angalau akapate ile fursa anayoitamani ya kuwa Mkuu wa Malaika Mbinguni.
AHSANTE
MHE.MSIGWA
0 maoni: