![]() |
| Advertisement |
Ikiwa ni siku moja baada ya Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe kulitupia mzigo wa lawama Jeshi la polisi kwa kuwa shikilia wahanga wa Mabomu waliokamatwa na jeshi hilo february 16, 2018
Leo Aida Olomi, Isaack lomanus, na Erick John Majeruhi wa Risasi Waliokuwa Wanashikiliwa na Jeshi la polisi Wamefikishwa Mahakama ya Kisutu .Ambapo Wamesomewa Mashtaka yao na Wameachiwa kwa Dhamana.
Wakili Alex Masaba anaripoti kwamba, Aida Ulomi na wenzake wawili wamepata dhamana mida hii katika Mahakama ya Kisutu
Kwa sasa Aida na wenzake wanafanyiwa utaratibu wa kupata matibabu ya jeraha waliopata kutokana na risasi.
Hata hivyo Mbunge wa Jimbo la Ubungo Said Kubenea ameendelea kusisitiza uwepo wa tume huru kwa ajili ya uchunguzi wa matukio haya.
Wafuasi hao walijeruhiwa na walikamatwa na Jeshi la polisi ijumaa tar 16 February 2018 Siku moja kabla ya kufanyika uchaguzi wa jimbo la kinondoni ambapo Jeshi La polisi lilikuwa likizima maandamando ya yaliyofanywa chama cha demokrasia na maendeleo chadema


0 maoni: