Jumanne, 27 Februari 2018

Viongozi wa Chadema waachiwa kwa dhamana

ad300
Advertisement

Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo chadema mheshimiwa Freeman Mbowe baada ya kumaliza Mkutano wake Na waandishi wa habari leo aliwasili  katika kituo cha cha polisi Leo akiongozana na viongozi wengine wa chadema
Ambao ni  pamoja na naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).
Pia wakiwemo viongozi wa baraza la wanawake chadema (BAWACHA)Halima Mdee ambae ni Mwenyekiti na Muweka hazina wa chama hicho Esther Matiko

Lakini pia viongozi wengine ni mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, John Hech

Viongozi hao walifika kituoni hapo leo Jumanne Februari 27, 2018 na kuachiwa saa 1:02 usiku, kuitikia wito wa polisi.

Mmoja wa mawakili wa viongozi hao, Frederick Kihwelo ameeleza kuwa wote wameachiwa kwa dhamana kwa kutakiwa kuwa na mdhamini mmoja na kutakiwa kuripoti tena kituoni hapo Machi 5, 2018 saa 1 asubuhi.

Amesema viongozi hao walianza kuhojiwa saa 8:30 mchana, baada ya kufanya mazungumzo ya tuhuma zinazowakabili.

Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema akiwamo Mbowe.

Wito huo ulikuja siku chache baada ya kumalizika kwa uchaguzi katika jumbo LA kinondoni na baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi  akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo kwa mawakala wao

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji  hakwenda polisi kwa kuwa yupo nje ya nchi

Kabla ya kuwasili kituoni hapo Mwenyekiti Freeman Mbowe aliieza waandishi wa habari kwamba yeye na viongozi wengine watawasili polisi hii Leo

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: