Jumatano, 28 Februari 2018

Ni siku ya 100 sasa yuko wapi Azory?

ad300
Advertisement

Na Ibrahim chawe

Tarehe 30 November 2017 uongozi wa gazeti La Mwananchi ulipokea taarifa ya kupotea kwa Mwandishi wake wa kujitegemea wa Mkoani Pwani ndg Azory Gwanda  Mkewe aliuambia uongozi wa Mwananchi kuwa tar 21 november 2017 watu wanne waliokuwa katika gari aina ya Toyota land cruiser  nyeupe walifika katikati ya mji wa kibiti ambako ndio Azory anakokaa na kufanya shughuli zake Mara zote Na kumchukua.

Baada ya kumchukua Azory majira kama ya SAA nne Asubuhi gari hilo lilielekea shambani ambako Azory alimkuta mkewe Anna akiwa shambani na kumuomba ufunguo wa nyumba yao huku akieleza kuwa anasafari ndefu hivyo asingeweza kurudi Siku  hiyo.

Baada ya hapo gari lilirudi kinyume nyume hadi njia panda ya kuelekea nyumbani kwa Mwandishi huyo

Baada ya kurudi nyumbani Mke wa Mwandishi huyo aligundua ya kuwa nyumba yao ilikuwa imepekuliwa maana vitu vilikuwa vimepangalanyika 

Toka Siku hiyo Mwandishi Azory gwanda hakuonekana na Namba zake hazikupatikana

Siku chache baadae jeshi la polisi kupitia kamanda Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi lilisema kuwa uchunguzi kuhusu kupotea kwa Mwanahabari wa kujitegemea wa gazeti la Mwananchi, Azory Gwanda unaendelea.

Na lilihitaji  mtu yeyote mwenye taarifa au atakayesikia kuhusiana na mwandishi huyo asisite kulifahamisha jeshi hilo.

Wafanyakazi wa Mwananchi communication hii Leo  wakihotubia waandishi wa habari ikiwa no  siku ya 100 tangu mfanyakazi mwenzao Azory Gwanda kupotea.

Francis Nanai Mkurugenzi Mtendaji wa MCL amesema wataisaida familia ya mwandishi huyo kwa kulipia ada za watoto,bima ya afya na mtaji wa kujikimu kiuchumi.

Mpaka sasa MCL hawana ripoti yoyote toka chombo chochote juu ya kupotea Kwa Azory.

Mara ya Mwisho Azory aliwasiliana na ofisi ya Mwananchi Tarehe 20 November 2017 kuhusu majukumu ya kikazi

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: