![]() |
Advertisement |
Kikosi cha Mbao ambacho wiki iliyopita kimeondoshwa katika michuano ya Azam sports federation cup maarufu kama kombe la shirikisho
leo kipo Dar es salaam kusaka pointi tatu Muhimu dhidi ya simba zitakazo wawezesha kuwa nafasi nzuri katika msimamo wa ligi kuu
kabla ya mchezo huo Mbao fc wamepeleka salaamu kwa wapinzani wao kuelekea mchezo huo utakaopigwa Leo jumatatu katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam na kusema kuwa wamekuja kupata ushindi na si vinginevyo.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Solly Zephania Njashi, alisema kuwa maandalizi yao ya mchezo wa leo yapo vizuri na wamejiandaa vya kutosha na wamekuja kwa ajili ya kupata ushindi.
“Sisi tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wetu wa kesho (leo) na mashabiki wafike kwa wingi kwani tuna uhakika tutaibuka na ushindi, tumejipanga kuhusu hilo.
“Sisi tumekuja kupata ushindi, siyo kupoteza, sema tatizo huwezi jua naye mpinzani wako amejipanga vipi kwenye mchezo huo, lakini sisi tupo vizuri na kikosi hakina majeruhi, bali kuna mmoja tu ambaye tulimpandisha kutoka kwenye academia, ila mwalimu atatoa ripoti kama atacheza au la"
Ikumbukwe kuwa Mbao fc wanashika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara huku simba akiwa nafasi ya kwanza katika msimamo huo
0 maoni: