![]() |
Advertisement |
Uongozi wa Yanga umetangaza viingilio vya mechi dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia itakayopigwa kesho, Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa huku bei ya mzunguko ikiwa ni Sh3000.
Taarifa iliyotolewa na Yanga katika mtandao wake inaonyesha kwamba VIP A kiingilio kitakuwa 15,000, VIP B na C itakuwa 10,000.
Kikosi cha Waethiopia kilitua jijini Dar es Salaam juzi Jumatano mchana na kimeendelea na mazoezi yake kujiandaa na mchezo huo.
Hata hivyo, mashabiki wa Yanga waliandika kwenye mtandao wa Instagram wakiuomba uongozi wa klabu hiyo kupunguza kiingilio kama ilivyokuwa kwa Taifa Stars ambapo walilipa Sh1,000 kwa jukwaa la mzunguko.
Aidha, uongozi wa Yanga umeendeleza kampeni ya mtandaoni ya kuwahimiza mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Taifa kesho.
Baadhi ya picha ambazo zilisambaa mtandaoni zilikuwa na ujumbe unaoeleza kwamba ‘Uwanjani kwanza mambo mengine baadaye
0 maoni: