![]() |
Advertisement |
Hii Leo mawaziri wa wizara mbalimbali za serikali wanajibu hoja na kupokea mapendekezo yaliyotolewa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali CAG mawaziri ambao watatoa majibu ni pamoja Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk Phillip Mpango
Ambae kwa upande wa wizara yake amesema Serikali imemchukulia hatua mhusika katika suala la ubadhirifu wa fedha ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji.
Dk Mpango alikuwa akijibu hoja zilizoibuliwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, (CAG) Musa Assad ambaye alibainisha ubadhirifu katika ubalozi wa Tanzania uliopo Maputo nchini humo.
“Tayari (Serikali) imemchukulia hatua mhusika na taratibu za kimahakama zinaendelea, dhumuni ni kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa,”amesema Dk Mpango
Mawaziri hao wanazungumza baada ya ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Asad kuanika upungufu unaogusa wizara zao jana bungeni.
Awali, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Seleman Jafo amezungumza na kujibu hoja za ripoti hiyo.
Hata hivyo, kwa leo wamezungumza mawaziri wawili na kesho wataendelea wengine hadi Jumapili wiki hii.
Mawaziri zaidi ya watano walikuwepo katika mkutano wa leo kujibu hoja zilizoibuliwa na ripoti ya CAG.
0 maoni: