Jumanne, 24 Aprili 2018

Hakielimu yaiomba serikali kuwekeza katika miundombinu ya Elimu

ad300
Advertisement

Taasisi ya HakiElimu yaiomba Serikali kuwekeza zaidi katika miundo mbinu ya elimu hapa nchini. Tathimini ya miundo mbinu ya elimu inaonyesha upungufu wa maktaba katika shule za msingi umeongezeka kutoka 88% ya mwaka 2016 hadi 91% mwaka 2017.

Shirika la HakiElimu leo latoa mapendekezo 7 ya kupewa kipaumbele katika sekta ya elimu. Miongoni mwa vipaumbele hivyo ni kutatua changamoto za kibajeti zinazohusiana na ajira za walimu, elimu ya mtoto wa kike, na bajeti kwa ajili ruzuku za wanafunzi (capitation grant).
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa shirika la haki elimu bwana John kalage amesema kuwa

Katika kipindi cha miaka 3 mfululizo tumeshuhudia bajeti ya elimu ikishuka kwa takribani 1% kila mwaka. Ili tuweze kuboresha elimu hapa nchini tunahitaji tuwekeze vya kutosha katika miundo mbinu. Angalau Serikali iwekeze kwa 20% -

Katika mwaka wa fedha 2017/18, bajeti ya Wizara ya Elimu kwa ajili ya miradi ya Maendeleo ilikua ni Sh. 916.8 bilioni. Hadi kufikia mwezi Machi 2018, kiasi cha shilingi 595.6 bilioni sawa na 65% tu ndiyo fedha iliyotolewa .

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: