Jumanne, 13 Machi 2018

Janjaro:nitaongeza mke wa pili

ad300
Advertisement

Msanii wa muziki Bongoflava. Dogo Janja amefunguka mipango yake ya kuoa mke wa pili.Dogo Janja ambaye alimuoa Irene Uwoya mwaka jana ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa kuoa mke wa pili hadi wa nne ni moja ya mipango yake na atafanya hivyo kila baada ya miaka 10.

“Inshallah kuongeza wa pili, wa tatu, wa nane hapo ukishakaa vizuri kiuchumi na mwenzako aweze ameridhia,” amesema.

“Hata wanne sio mbaya hapo tunaongelea Mwenyenzi Mugu akitujalia uhai labda baada ya miaka 10 naweza kuongeza wa pili, ikifika miaka 10 tena naongeza, yaani nikifika miaka 50 pale niwe nimekamilisha wanne,” ameongeza.

Dogo Janja na Irene Uwoya waliripotiwa kufunga ndoa November 25, 2017, hata hivyo ni vigumu kutaja tarehe kamili kutokana na namna walivyoliweka suala hilo hasa kwa upande wa vyombo vya habari na mitandao.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: