Jumatatu, 26 Februari 2018

Serikali ya Nigeria kuwasaka Mabinti waliopotea

ad300
Advertisement

Serikali ya Nigeria imethibitisha kwamba wasichana 110 wa Chuo cha Ufundi bado hawajulikani walipo baada ya shambulio lililofanywa na Boko Haram wiki iliyopita kaskazini mashariki mwa jimbo la Yobe.

Idadi hiyo ilithibitishwa na Waziri wa Habari na Utamaduni Lai Mohammed baada ya kukutana na wazazi, mashirika ya usalama na wawakilishi wa serikali za mitaa ambao walikusanyika katika mji mkuu wa Jimbo la Yobe, Damaturu kujadili tukio la Jumatatu iliyopita katika Chuo cha Ufundi kwa Wasichana, katika eneo la Dapchi .

"Kati ya wanafunzi 906 walioandikishwa siku hiyo wanafunzi 110 hawajulikani walipo,” alisema Mohammed.
Ofisa huyo alisema hakuna jiwe litakaloachwa bila kubinuliwa kwani serikali imedhamiria kumwokoa kila mwanafunzi aliyepotea.

Katika taarifa yake Ijumaa, kiongozi wa Nigeria Muhammadu Buhari alielezea tukio hili kama "janga la taifa," akisema "nchi nzima inashikamana na familia za wasichana."

Janga la kupotea kwa wasichana hao limerejesha kumbukumbu za tukio kama hilo lililotokea miaka minne iliyopita wakati zaidi ya watoto wa shule 200 pia kutoka ya wasichana tu, walipotekwa na Boko Haram katika mji wa kaskazini mashariki mwa Chibok.

Kundi la Boko Haram ambalo limepigwa marufuku limekuwa likijaribu kuanzisha tangu 2009 taifa la Kiislamu kaskazini mashariki mwa Nigeria. Wameua watu wapatao 20,000 na mamilioni ya watu wengine wametawanyika.

Katika hatua nyingine serikali imesema kwamba imeongeza nguvu ya ndege za kivita ili kuendesha msako wa wasichana hao.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: